Tarehe : Dec. 24, 2018, 10:15 a.m.
Na Greyson Mwase, Dodoma
Leo tarehe 21 Desemba, 2018 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ameongoza kikao cha kazi cha Tume ya Madini kilichofanyika jijini Dodoma. Kikao hicho kilishirikisha makamishna wa Tume ambao ni Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Nchini (FEMATA), Haroun Kinega, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa.
Wengine ni Dkt. Athanas Macheyeki, Profesa Abdulkarim Mruma Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya pamoja na watendaji wa Tume ya Madini.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Tume na Mpango Mkakati wa Tume wa miaka mitano (2019/20 -2023/2024). Katika kikao hicho kati ya masuala yaliyokubaliwa ni pamoja na leseni ambazo hazifanyiwi kazi kufutwa na tathmini ya kina kufanyika kwa waombaji wa leseni ili kubaini kama wanakidhi vigezo kama vile uwezo wa kifedha na utaalam.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.