[Latest Updates]: Ujumbe Kutoka Umoja wa Uwazi na Uwajibikaji (EITI) Wakutana na Kampuni za Madini na Gesi

Tarehe : April 5, 2024, 10:01 p.m.
left

Dar es salaam. 

Ujumbe kutoka Asasi ya Umoja wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (EITI) ukiongozwa Katibu Mtendaji  Mr. Mark Robinson na  umekutana na wawakilishi wa Kampuni za Madini na Gesi na mashirika ya Umma ya TPDC na Stamico kujadili utekelezaji wa shughuli za EITI nchini. 

Maeneo yaliyolengwa katika majadiliano hayo ni ushiriki wa kampuni na mashirika ya Umma (State Owned Enterprises -SOEs) yanayofanya shughuli za Uziduaji katika utekelezaji wa vigezo vya Kimataifa vya Uwazi na Uwajibikaji vya mwaka 2023 ( EITI Standard 2023) Aprili 4, 2024 jijini Dar es Salaam.

Mapitio ya matokeo ya Tathmini (Validation) ya mwaka 2023 ambapo masuala yafuatayo yalipendekezwa kuboreshwa ili Tanzania ifanye vizuri katika Tathmini ijayo ya mwaka 2027, uwekaji wazi wa mikataba ya Madini na Gesi Asilia na uwekaji wazi wa Wamiliki wanufaika (Beneficial Owners) katika kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia.

Mchango wa wachimbaji wadogo na urasimishaji wa sekta ya uchimbaji mdogo.

Ushiriki wa kampuni na SOEs katika utekelezaji wa vigezo vipya vilivyoongezwa   (EITI Standard 2023). Vigezo hivyo ni pamoja na masuala ya kuzuia rusha, jinsia na mazingira na Energy Transition.

Aidha, katika majadiliano hayo, ilielezwa kuwa baadhi ya kampuni tayari zimeweka wazi mikataba yake kupitia masoko ya hisa na hivyo iko wazi kwa Umma pia ilielezwa kuwa uwekaji wazi tayari mikataba  utasaidia kuhamasisha Uwazi na wananchi kujua faida  kutoka katika uvunaji wa rasilimali madini Mafuta na  Gesi. Wawakilishi watatoa ushirikiano kwa Sekretariati ya  EITI Tanzania katika utekelezaji wa vigezo vya Kimataifa vya mwaka 2023.

Pia, Wawakilishi wa kampuni na mashirika yafuatayo walihudhuria. Pan Africa Energy, Maurel & Prom, Tanzania Chamber of Mines, Tembo Nickel, Shanta Gold Mine, TPDC na Stamico.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals