[Latest Updates]: Wizara ya Madini Kukutana Kila Mwezi Kujadili Maendeleo Sekta ya Madini

Tarehe : Oct. 7, 2023, 9:16 a.m.
left

 

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde ameongoza kikao cha Watendaji wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini yake ikiwa ni utaratibu ulioanzishwa wa kukutana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kujadiliana utekelezaji wa majukumu, miradi pamoja na kufahamishana hatua mbalimbali zilizofikiwa katika Sekta ya Madini na masuala yanayohusu changamoto na maendeleo ya Sekta kwa ujumla.

Kikao hicho cha leo Oktoba 7, 2023, pia kimejadili na kutafakari ikiwemo kuweka mikakati  itakayoongeza ushiriki wa Watanzania hususan vijana na wanawake katika Sekta ya Madini pamoja na kuongeza tija na thamani ya Sekta kwenye uchumi wa nchi na hatimaye mchango Pato la Taifa.

Mhe. Mavunde amerejelea kuhusu uwepo wa mpango mpya unaoitwa Madini kwa kesho bora (Mining for Brighter Tomorrow -MBT) ukiwa na lengo la kuwasaidia vijana, wanawake pamoja na wahitimu wa vyuo vikuu kunufaika kupitia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini,  Kheri Mahimbali amesema  vikao hivyo vitasaidia kuifungua fursa kwa Watendaji wa Wizara na Wakuu wa Taasisi kutoa mawazo yao kwa kuwa vinajadili masuala muhimu na makubwa kuhusu Sekta ya Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals