[Latest Updates]: STAMICO Yatoa Elimu ya Matumizi ya Rafiki Briquette kwa Jeshi la Magereza

Tarehe : Sept. 18, 2024, 11:50 a.m.
left

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetoa mafunzo ya siku moja kuwajengea uwezo Maafisa na Watendaji wengine wa Jeshi la Magereza kuhusu matumizi bora ya nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquette.

Mafunzo hayo yamefanyika Septemba 18,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kamishna wa Huduma za Urekebu Jeshi la Magereza CP. Bertha Minde amefungua mafunzo hayo kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Jeremiah Yoram Katungu.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo CP. Minde amesema, Jeshi la Magereza limeandaa Programu ya Matumizi ya Nishati safi ya kupikia ambayo ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati hiyo  kwa Mwaka 2024 hadi 2034 na maelekezo ya Mhe.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu Taasisi zenye idadi ya watu zaidi ya 100 kuachana na Matumizi ya kuni na kuanza kutumia Nishati safi katika kuandaa chakula.

Aidha CP. Minde amesema pamoja na vyanzo vingine vya Nishati safi ya kupikia, Jeshi la Magereza linatarajia kutumia Mkaa mbadala wa Rafiki Briquette kama chanzo kikuu cha nishati safi ya kupikia Magerezani.

Kwa upande wake,Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Bw. Gabriel Nderumaki amesema Ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na STAMICO unalenga kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali na kuangalia fursa zilizopo katika Taasisi hizi Mbili na kuzitumia Kwa manufaa ya Taasisi na Taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa mkaa wa Rafiki Briquette ni nishati bora ambayo imethibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na gharama yake ni nafuu ambayo kila mwananchi na taasisi zinaweza kumudu.

Katika mafunzo hayo,STAMICO pia ilionyesha kwa vitendo jinsi ya kutumia nishati ya Rafiki Briquette na washiriki waliridhika na ubora wake.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals