[Latest Updates]: Serikali yaainisha Mpango wa Kusaidia Wachimbaji Wadogo Nchini

Tarehe : May 9, 2024, 1:12 p.m.
left

Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde ameainisha mpango wa Serikali wa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Mei 9, 2024 wakati akijibu swali la Mhe. Dkt. Christine  Ishengoma Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga.

Ameongeza kwamba, mpango wa Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo wachimbaji wa madini wa Wilaya ya Ulanga unahusisha masuala mbalimbali ikiwemo 
Kuwekeza zaidi katika utafiti wa kina kugundua uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo.

“ Mhe. Spika maeneo mengine ni utoaji wa leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo; kutoa elimu ya matumzi ya teknolojia sahihi ya uchimbaji ili kuongeza tija; huduma ya uchorongaji kwa gharama nafuu kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),” amesema Waziri Mavunde.

Vilevile, amesema kuwa, mpango mwingine ni kuwezesha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wachimbaji; na fursa ya ukodishaji wa mitambo na vifaa chini ya usimamizi wa STAMICO.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals