[Latest Updates]: Wabunge wa Afrika Kusini wajifunza uzoefu sekta ya madini Tanzania

Tarehe : June 20, 2018, 11:54 a.m.
left

Kamati ya Jamii na Masuala ya Usalama ya Bunge la Jimbo la Ghanteng, Afrika Kusini, wametembelea Wizara ya Madini kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu namna sekta husika inavyoendeshwa nchini.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki (mwenye nguo ya kitenge), Naibu Mawaziri wa Madini Stanslaus Nyongo (kushoto kwa Waziri) na Doto Biteko (kulia kwa Waziri), wakibadilishana mawazo na Wajumbe wa Kamati ya Jamii na Masuala ya Usalama ya Bunge la Jimbo la Ghanteng, Afrika Kusini, waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dodoma, Juni 19, 2018 kujifunza na kupata uzoefu namna sekta husika inavyoendeshwa nchini.[/caption]

Wawakilishi hao wa wananchi wa Afrika Kusini, walipokelewa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki, Naibu Mawaziri Doto Biteko na Stanslaus Nyongo pamoja na Katibu Mkuu Prof Simon Msanjila, jana Juni 19, 2018, Makao Makuu ya Wizara Dodoma.

Akizungumzia nia ya ujio wao, Kiongozi wa Ujumbe huo ambaye ndiye pia Mwenyekiti wa Kamati husika, S. Khanyile alisema kuwa, walipenda kupata uzoefu wa Tanzania katika kusimamia uchimbaji mdogo wa madini pamoja na mbinu za udhibiti wa uchimbaji haramu wa madini.

Akiwasilisha Mada kwa Ujumbe huo kuhusu maeneo husika; Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi David Mulabwa, alieleza kuwa, katika kusimamia uchimbaji mdogo, Serikali kupitia Wizara ya Madini inatekeleza mambo kadhaa muhimu ambayo ni pamoja na kuhakikisha wachimbaji wote wanarasimishwa kwa kupatiwa leseni.

Kamishna Mulabwa alieleza kuwa, pamoja na kuwarasimisha wachimbaji, Serikali pia inatoa mafunzo mbalimbali kwao kwa lengo la kuwajengea uelewa, inatenga maeneo ya uchimbaji kwa ajili yao pamoja na kujenga vituo vya mfano kama vile Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa ambao pia utakuwa na Mtambo wa Uchenjuaji madini.

“Vilevile, tunasimamia pia suala la makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali stahiki kutoka kwa sekta hii ya uchimbaji mdogo. Ili suala hili liwe na mafanikio, ni lazima kuhakikisha wachimbaji wanawezeshwa ipasavyo kupitia mafunzo na mambo mbalimbali kama nilivyoeleza awali,” alifafanua.

Aidha, aliongeza kuwa, Serikali imekuwa ikiwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwapatia ruzuku lakini akabainisha kuwa utaratibu huo umesitishwa kwa muda baada ya kujitokeza changamoto kadhaa, na utarejeshwa tena baada ya kuaandaa utaratibu mzuri zaidi na wenye tija katika kuendesha zoezi hilo.

Kuhusu suala la udhibiti wa uchimbaji haramu wa madini, Mhandisi Mulabwa alieleza kuwa, Tanzania imeweka mfumo mzuri wa kisheria ambao unamtaka yeyote anayejishughulisha na uchimbaji madini kuwa na leseni halali.

Wajumbe wa Kamati ya Jamii na Masuala ya Usalama ya Bunge la Jimbo la Ghanteng, Afrika Kusini, waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dodoma, Juni 19, 2018 kujifunza na kupata uzoefu namna sekta husika inavyoendeshwa nchini; wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi David Mulabwa (hayupo pichani).[/caption]

Alisema kuwa, Serikali pia imeweka utaratibu wa kusimamia kwa karibu shughuli zote za uchimbaji ikiwemo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.

Vilevile, alisema kuwa kuimarisha mawasiliano kuanzia ngazi ya chini yaani Serikali ya Kijiji, Wilaya na hatimaye Ofisi za Madini ni muhimu sana katika udhibiti wa uchimbaji haramu.

“Kupitia mawasiliano hayo tunafanikiwa kupata taarifa zote mara moja na hivyo inatusaidia kuchukua hatua stahiki na kwa wakati stahiki.”

Kwa upande wake, Waziri Kairuki aliwashukuru wabunge hao kwa kufanya uamuzi wa kuja kujifunza Tanzania na kuomba ushirikiano baina yao uendelezwe. Wabunge hao pia walishukuru kwa ushirikiano waliopata na kusema kuwa wamefurahi kupata uzoefu wa Tanzania ambao utawasaidia katika uboreshaji wa sekta hiyo nchini kwao.

Imeandaliwa na:

Veronica Simba na Samwel Mtuwa, Dodoma

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

Kikuyu Avenue,

P.O Box 422,

40474 Dodoma,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

BaruaPepe: info@madini.go.tz,                                             

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals