[Latest Updates]: Ujumbe kutoka Kenya wajifunza Usimamizi Sekta ya Madini

Tarehe : July 24, 2023, 4:56 p.m.
left

Ujumbe kutoka Kenya ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini wa nchi hiyo Elijah Mwangi umefika nchini kujifunza kuhusu namna bora ya usimamizi wa Sekta ya Madini ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali ameupokea ujumbe huo.

Akizungumza katika kikao na ujumbe huo, Mahimbali amesema Tanzania ni sehemu salama ya uwekezaji kutokana na uongozi bora wa Serikali unaosimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo umepelekea kuifanya sekta hiyo kupata mafanikio makubwa.

Mahimbali amesema Wizara ya Madini ina Taasisi tano ambazo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) pamoja na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) ambazo hutekeleza majukumu yake kwa ushirikiano.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Uchumi wa Bluu kutoka Kenya Elijah Mwangi ameipongeza Wizara ya Madini kwa usimamizi bora wa sekta hiyo na kumuomba Mahimbali kuendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo tafiti na usimamizi wa biashara ya madini.

Katika kikao hicho mada mbalimbali zimewasilishwa ambapo Mtendaji Mkuu wa  GST Dkt. Mussa Budeba amewasilisha mada juu ya madini yapatikanayo Tanzania na aina za tafiti zilizokwisha fanyika. 

Dkt. Budeba amesema kwa sasa GST imejikita zaidi kwenye tafiti za madini ya kimkakati ambapo mpaka sasa Tanzania imefanyiwa tafiti za Kijiolojia kwa asilimia 96.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Ally Maganga amewasilisha mada juu ya shughuli za Tume ya Madini ikiwemo uwepo wa Masomo na Vituo vya Ununuzi wa Madini, Mfumo wa Leseni pamoja na shughuli za wachimbaji wadogo.

Mhandisi Maganga amesema   uwepo wa masoko na vituo vya kuuzia madini umesaidia kuongeza mapato ya Sekta ya Madini ambapo mchango wa sekta hiyo kwenye Pato la Taifa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo kwa sasa umefikia asilimia 9.7 ikiwa lengo ni kufikia mchango wa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals