[Latest Updates]: Mafunzo kuhusu mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato (GePG) yatolewa kwa wahasibu wa Madini

Tarehe : Nov. 12, 2018, 8:53 a.m.
left

Na Rhoda James, Morogoro                                                                                                                                          

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Tume ya Madini kufuatilia madeni yote ya ada ya mwaka (Annual Rent) na kutoa muda kwa wahusika ili walipe ada hizo na endapo watashindwa kulipa katika muda watakaopewa, wapelekwe Mahakamani.

Naibu Waziri wa Madani, Doto Biteko (kushoto) mara baada ya kusaini kitabu cha wangeni katika Ofisi ya Mratibu wa Chuo cha Mazimbu Campus Solomn Maalangu Dkt. Ibrahimu Mjema mkoani Morogoro.[/caption]

Naibu Waziri Biteko ameyasema hayo Novemba 12, wakati akifungua mafunzo ya Wahasibu wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini kutoka maeneo mbalimbali nchini wanaohudhuria mafunzo hayo yanayohusu Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki katika Ukusanyaji wa Mapato (Goverment E- Payment Gateway – GePG). Mafunzo hayo yanafanyika  katika chuo cha Mazimbu Campus Solomn Mkoani Morogoro.

“Serikali inadai madeni mengi ya ada za mwaka, mfano kuna mtu moja ana leseni 103 na anaendela kuomba leseni nyingine lakini pia huyo mtu anadaiwa pesa nyingi za ada ya mwaka,” amesema Biteko.

Naibu Waziri Biteko amesisitiza kuwa lengo la mfumo huo ni kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kupunguza mianya ya upotevu wa mapato kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi zote za Serikali.

Pia, Naibu Waziri Biteko ameongeza kuwa, ili kuleta tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, Mfumo wa GePG umeunganishwa na taasisi zinazotoa huduma za fedha kama vile Simu Benking za NMB na CRDB pamoja na Kampuni za Simu ambazo zinatoa huduma kupitia matawi, mawakala na mitandao ya simu lengo likiwa ni kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kutumia mfumo huo.

Akifafanua zaidi, Naibu Waziri Biteko amesema kuwa mafunzo hayo yapo kisheria na yanatokana na kifungu cha 44 cha Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 (The Finance Act, 2017) ambapo Wizara iliunganishwa rasmi kwenye mfumo huo mwezi Septemba, 2017.

Naibu Waziri Madini Biteko ameongeza kuwa, mnamo tarehe 4 Septemba, 2017 Serikali ilitoa Waraka wa Hazina Na. 3 kuhusu kutumia mfumo wa Serikali wa Kielektroniki katika Ukusanyaji wa Mapato lengo likiwa ni kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuhusu kujengwa kwa mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato yote ya Serikali.

Wahasimu kutoka Wizara ya Madini nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani).[/caption]

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko amewapongeza Wahasibu wote kwa kufanikiwa kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 310 katika mwaka wa fedha 2018/19 na kueleza kuwa, mpaka kufikia tarehe 31 Oktoba, 2018 jumla ya maduhuli yenye thamani ya shilingi bilioni 111 yamekusanywa ambapo ni asilimia 36 ya lengo ambalo wizara iliwekewa  kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume, Prof. Shukrani Manya amesema kuwa, Mafunzo hayo ni muhimu kwa Tume ya Madini na kwamba yataleta fursa mbalimbali kama vile kujifunza na kuboresha utendaji wa wahasibu katika Tume ya Madini.

Mafunzo kama hayo yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo tarehe 28 hadi 31 Agosti, 2017. Kwa mwaka huu,mafunzo haya yameanza leo Novemba 12 na yanatarajia kukamilika tarehe 15 Novemba, 2018.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals