[Latest Updates]: STAMICO Kuendelea Kuwashika Mkono Wachimbaji wa Madini Vijana na Wanawake

Tarehe : July 12, 2024, 3:34 p.m.
left

Dkt. Mwasse azindua duka la Madini ya Vito la Wachimbaji Vijana (Vijana Gem Shop)

Vijana na Wanawake waoneshwa fursa katika uongezaji thamani madini

Leo Ijumaa tarehe 12.07.2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amezindua duka la madini ya Vito, Vijana Gem Shop duka lilipo Upanga, Dar es Salaam na linalomilikiwa na Chama cha Wachimbaji Wanawake (TAWOMA).

Hafla ya Uzinduzi umefanyika katika Ofisi ya TAWOMA, Jengo la STAMICO Mtaa wa Undali Jijini Dar es Salaam.

Katika Hotuba ya ufunguzi Dkt. Mwasse ameeleza uwepo wa fursa mbalimbali kwenye sekta ya Madini kuanzia kwenye uchimbaji hadi kwenye uongezaji thamani. 

Ameongeza kuwa kupitia Malengo Endelevu (SDG) ambayo yanasisitiza Uwezeshaji Wanawake(Women Empowerement), Usawa wa Kijinsia  (Gender Equity) na Maendeleo Endelevu (Sustainable Development) na Maendeleo Jumuishi (Inclusive Development) vijana na Wanawake wanayo fursa kubwa ya kunufaika na Rasilimali Madini kwa kushiriki kwenye shughuli za Uchimbaji na Uongezaji thamani. 

Aidha, Dkt. Mwasse amewataka pia Taasisi za fedha (Mabenki) kuwezesha shughuli za uchimbaji na uongezaji thamani hususani madini ya vito na madini ya viwandani kwani sekta hii inakua kwa kasi na kuajiri watanzania wengi hususani Vijana na Wanawake.

Katika kuhitimisha hotuba yake 
Dkt. Mwasse amesema STAMICO iko tayari kushirikiana na Wabia wa Maendeleo wakiwemo PACT Tanzania, Beutfull Story na MOYO Gem na Taasisi za nyingine za kifedha kuboresha na kuwezesha Wachimbaji Wadogo Vijana na Wanawake ili waweze kunufaika na rasimali Madini. 

Kwa kufanya hivi tutakuwa tunaunga Mkono jitihada za Mhe. Dkt Samia Suluhu Hasan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongeza ajira nchini na kuwezesha sekta ya madini kuchangia vizuri kwenye Pato la Taifa, Alisema Dkt Mwasse.

Mkurugezi Mtendaji wa STAMICO amewapongeza TAWOMA - Youth kwa kuonesha mfano hususani kwenye shughuli za uongezaji thamani madini na Kufungua Duka la Madini (Vijana Gem Shop). Aidha ameupongeza uongozi wa TAWOMA chini ya Mwenyekiti wake Mama Semeni Malale (Iron lady) kwa ulipaji wa Kodi na Ada mbalimbali za Serikali na urudishaji faida kwa jamii (CSR).

Tukio hili la uzinduzi limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo rais wa FEMATA Bw. John Bina, Mhe. Emanuel Silanga (M-NEC), RMO Mkoa wa Dar es Salaam, Wawakilishi kutoka PACT, Benki, Makampuni ya Madini, DACOREMA, Umoja Trust (Uganda), Chemba ya Migodi, Tanzania Youth in Mine (TYM).

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals