[Latest Updates]: Prof. Msanjila akutana na kamati ya maandalizi uzinduzi wa ukuta Mirerani na Wadau wa madini

Tarehe : March 20, 2018, 8:33 a.m.
left

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini , Profesa Simon Msanjila leo tarehe 18 Machi, amekutana na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi wa Ukuta unaozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite  Mirerani, Wilayani Simanjiro.

Ukuta huo unatarajiwa  kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli mapema mwezi Aprili.

Kikao hicho kimewashirikisha Watumishi kutoka Wizara ya Madini, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Makamanda kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Akizungumza katika kikao hicho Prof. Msanjila amelipongeza Jeshi kwa ujenzi wa kasi wa ukuta huo  na kuongeza kuwa ilikuwa ni kazi ya kujitolea na jeshi limeisimamia vizuri.

Kwa upande wake, Naibu Kamanda wa Oparesheni ya ujenzi wa ukuta huo, Luteni Kanali Rashidi Kanole amesema kuwa, siri ya  ujenzi wa ukuta kuchukua muda mfupi tofauti na muda wa utekelezaji wake,  pamoja na mambo mengine umetokana na  kufanya kazi kwa kuzingatia utamaduni wa jeshi unaohusisha kiapo na uzalendo na kutafuta mbinu za changamoto bila kusubiri viongozi wa juu kwenda kutatua changamoto hizo.

Ujenzi wa ukuta huo ulipangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi sita lakini umekamilika ndani ya kipindi cha miezi 3.

Sambamba na kikao hicho,  pia, Prof. Msanjila amekutana na wadau wa madini wilayani humo kujadili masuala mbalimbali kuhusu  biashara ya madini hayo mara baada ya ukuta wa kuzinduliwa.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na ulinzi shirikishi wa ukuta huo, biashara ya Tanzanite, uwazi wa biashara na suala la vitambulisho vya Taifa.

Kuhusu vitambulisho Prof. Msanjila amesema kuwa atakayeingia  ndani ya ukuta huo ni yule tu atakayekuwa na kitambulisho cha Taifa.

Aidha, pande zote mbili Serikali na  wadau wamekulllliana kukutana tena illlmujadili kwa kina  suala la biashara ya madini hayo mara baada ya ukuta kuzinduliwa.

Imeandaliwa na:

Asteria Muhozya,

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@madini.go.tz,                                                                               

Tovuti: madini.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals