Tarehe : Oct. 7, 2022, 11:20 a.m.
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshiriki Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Madini Afrika uliondaliwa na Umoja wa Afrika na kufanyika Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Mkutano huo umelenga kujadili mkakati wa pamoja wa nchi za Afrika kuhusu ugunduzi, uendelezaji na uvunaji madini mkakati hasusan green energy minerals ambayo yanahusisha madini ya Lithium, Nickel, Copper, Graphite, Manganese, cobalt, Vanadium ambayo ni muhimu kwa nishati ya magari ya umeme, umeme wa solar, batteries aina zote, transformer za umeme kwa lengo la kupunguza kiwango cha carbon kwenye anga.
Maadini mengine ya kimkakati yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni madini teknolojia ambayo ni REE, PGE, Phosphate, Niobium Tin.
Aidha, masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuangalia Sera, Sheria na Kanuni zinazowezesha kuongeza manufaa kwa nchi za Afrika na wananchi wake kutilia mkazo suala la uongezaji thamani madini mkakati hadi zao la mwisho.
Vilevile, Serikali za nchi za Afrika zimehimizwa kujikita katika utafutaji madini badala ya kuziachia sekta binafsi haususan kampuni za kigeni pekee.
Mfano umetolewa kwa nchi ya Namibia ambayo Serikali yake kupitia Taasisi yake ya Jiolojia imefanikiwa kufanya utafiti wa madini nchi nzima ambapo hadi sasa Pato Kuu la Taifa hilo linategemea uchumi wa madini.
Mbali na hayo, mkutano huo umebainisha changamoto zinazozikabili nchi nchi za Afrika katika sekta hiyo kuwa ni kutokana na kuwepo kwa changamoto zinazotokana na uwezo mdogo wa mitaji, uwezo mdogo wa kufanya tafiti za madini na teknolojia ndogo ya kuongeza thamani madini.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri na Manaibu Waziri kutoka nchi za Tanzania, Zimbabwe, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Senegal, Sudani Kusini, Ethiopia, wawakilishi kutoka nchi za Namibia na Botswana pamoja na wadau wa sekta binafsi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira na utafutaji madini.
Katika mkutano huo, Dkt. Kiruswa aliongozana na Meneja wa Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Maswi M. Solomon
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.