[Latest Updates]: Nyongo awataka wachimbaji wadogo kuwajibika

Tarehe : April 28, 2018, 12:45 p.m.
left

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka wachimbaji wadogo wa madini nchini, kufahamu wajibu wao na kuutekeleza kikamilifu ili waendeshe shughuli zao kwa amani na tija.

Wananchi mbalimbali katika Migodi ya Nyakafuru, Musasa na Bingwa wakitoa maoni yao mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), wakati wa ziara yake katika maeneo hayo, Februari 26 mwaka huu. Naibu Waziri yuko katika ziara ya kazi kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa.[/caption]

Aliyasema hayo Februari 26 mwaka huu, alipotembelea na kuzungumza na wachimbaji wadogo wa Lwamgasa, Bingwa, Musasa na Nyakafuru katika Wilaya za Mbogwe na Chato, Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kazi inayoendelea Kanda ya Ziwa.

“Msiishie kulalamika tu. Jifunzeni kuwajibika kikamilifu katika nafasi zenu ili kazi zenu zilete tija na kuwanufaisha ninyi wenyewe, jamii na Taifa kwa ujumla.”

Alisema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya uongozi mahiri wa Rais John Magufuli, inawajali na kuwathamini sana wachimbaji wadogo lakini pia inawataka wawajibike ili mchango wao katika sekta husika uonekane.

Akifafanua zaidi, Naibu Waziri aliwataka wachimbaji hao kuhakikisha wanarasimisha shughuli zao kwa kuomba leseni ili wasajiliwe na kutambuliwa rasmi na Serikali, hivyo waweze kulipa kodi na tozo mbalimbali.

“Serikali inategemea kodi zenu ili iweze kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa Taifa ikiwemo kutoa elimu bure kama inavyofanyika sasa, kujenga miundombinu, kuwezesha utoaji wa huduma za afya na nyinginezo. Hivyo basi, ni lazima mlichukulie suala la uwajibikaji kwa umuhimu mkubwa,” alisisitiza.

Aidha, aliwasisitiza kuunda vikundi na kufanya shughuli zao ndani ya vikundi hivyo, ili iwe rahisi kwa Serikali kuwatambua na kuwapa huduma mbalimbali zitakazowasaidia kuboresha kazi zao.

Sehemu ya umati wa wananchi katika Machimbo ya Madini Bingwa, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), wakati wa ziara yake inayoendelea Kanda ya Ziwa kukagua shughuli za madini.[/caption]

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) John Bina, aliwasisitiza wachimbaji hao kujali afya zao na kuzingatia suala la kutumia vizuri mapato yao ili wajiletee maendeleo.

Naibu Waziri Nyongo anaendelea na ziara ya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Imeandaliwa na:

Veronica Simba, Geita

Afisa Habari,

Wizara ya Nishati na Madini,

Kikuyu Avenue,

P.O Box 422,

40474 Dodoma,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

BaruaPepe: info@mem.go.tz,                                             

Tovuti: mem.go.tz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals